Saturday, May 17, 2014

Kikosi cha TP Mazembe
Kikosi cha TP Mazembe
Klabu ya soka ya TP Mazembe ya nchini Congo jana imechezea kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa El Hilal Omdurani ya Sudan katika mchezo wa kwanza wa hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa barani Afrika.
El Hilal walianza kutibua mipango ya Mazembe katika dakika ya 51 baada ya Salah Al Jizoli kuandika bao la kuongoza kufuatia kumalizia pasi nzuri ya Bakri Babeker.
Kipigo hicho cha bao 1-0 kimewafanya Mazembe kuanza vibaya michuano hiyo na sasa watahitaji kufanya vizuri mchezoz unaofuata, huku wakiwa katika kundi A pamoja na wapinzani wao wakubwa AS Vita.
Washambuliaji wote wawili wa Tanzania wa TPM walicheza, Mbwana Samatta akianza na Thomas Ulimwengu akitokea benchi dakika ya 66 kwenda kuchukua nafasi ya Rainford Kalaba.
Samatta na Ulimwengu wanatarajiwa kuondoka asubuhi kuja Dar es Salaam kujiunga na timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars kwa ajili ya mchezo wa Jumapili dhidi ya Zimbabwe, kuwania hatua ya makundi ya kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Mataifa ya Afrika mwakani nchini Morocco

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog