Saturday, May 17, 2014


Rais wa shirikisho la kandanda ulimwenguni, FIFA, Sepp Blatter, amethibitisha ilikuwa kosa kuchagua Quatar kuwa mwenyeji wa kombe la dunia la mwaka wa 2022. Katika mahojiano na televisheni nchini Uswisi, Sepp Blatter aliulizwa iwapo kuiruhusu Qatar kuwa mwenyeji wa kombe hilo ambalo huchezwa kati ya mwezi Juni na Julai ilikuwa kosa, hasa ikizingatiwa kuwa hali ya hewa katika nchi hiyo hufikia hadi nyuzi joto 50 wakati huo. Alijibu kwa kukiri na kuongeza kuwa kila mtu hukosea maishani. Alipinga madai kwamba taifa hilo lilikuwa limelipia michezo hiyo. Aliongeza kuwa kamati inayojumuisha maafisa wa FIFA walikuwa wamekubali uwezekano wa taifa hilo kuwa mwenyeji ijapokuwa walikuwa wamepokea taarifa kuhusu vipimo vya juu vya joto. Alisema kwamba michezo hiyo badala yake inaweza kusogezwa hadi miezi ya mwisho wa mwaka, wakati vipimo vya joto vitakuwa vimepungua.

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog