Wednesday, August 6, 2014


Mgeni Rasmi katika uzinduzi wa albamu ya muziki wa Injili ,Waziri Mkuu mstaafu.Mh.Frederick Sumaye akionesha albamu ya mwanamuziki nyota wa muziki wa injili hapa nchini,Rose Muhando,iliyoitwa Shikilia Pindo la yesu,mara baada ya kuizindua rasmi mbele ya maelfu ya washabiki na wapenzi wa nyimbo hizo za kiroho ndani ya ukumbi wa Diamond Jubilee,jijini Dar jana.

Waziri Mkuu mstaafu.Mh.Frederick Sumaye akifungua kasha lenye CD, wakati akizundua rasmi albamu ya mwanamuziki nyota wa muziki wa injili hapa nchini,Rose Muhando,iliyoitwa Shikilia Pindo la yesu,uzinduzi huo umefanyika jana ndani ya ukumbi wa Diamond Jubilee na kuhudhuriwa na maelfu ya watu mbalimbali.Pichani kati ni Mkurugenzi wa Msama Promotions Ltd,Bwa.Alex Msama sambamba na Mwimbaji nyota wa Injili,Rose Muhando wakishuhudia tukio hilo.

Uzinduzi huo ulioandaliwa na kampuni ya Msama Promotions,ulionekana kufana kwa kwa kiasi kikubwa,huku waimbaji balimbali wakiwa wameshiriki onesho hilo,lililokonga washabiki na wapenzi wa muziki huo kwa kiasi kikubwa.


Waziri Mkuu mstaafu.Mh.Frederick Sumaye akisalimiana na mwanamuziki nyota wa muziki wa injili hapa nchini,Rose Muhando,iliyoitwa Shikilia Pindo la yesu,uzinduzi huo umefanyika jana ndani ya ukumbi wa Diamond Jubilee na kuhudhuriwa na maelfu ya watu mbalimbali.

Baadhi ya Wadau wa Muziki wa Injili wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye uzinduzi huo uliofana kwa kiasi kikubwa.

Sehemu ya umati ya watu waliofika kwenye uzinduzi huo

Mwimbaji wa nyimbo za Injili,Rose Muhanda akiwa na skwadi lake jukwaani wakiimba mbele ya umati mkubwa wa watu (hawapo pichani),wakati wa uzinduzi wa albamu yake mpya,uliofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee hapo jana,ambapo mgeni rasmi alikuwa Waziri Mkuu Mstaafu,Mh Frederick Sumaye.

Rose Muhando akiimba kwa hisia

Sehemu ya umati wa watu waliohudhuria uzinduzi huo

Mwimbaji wa nyimbo za Kiroho,Upendo Kilahilo,akiimba jukwaani.

Mwimbaji wa nyimbo za Injili kutoka nchini Kenya,Sara K akiimba


Waziri Mkuu Mstaafu,Mh Frederick Sumaye na wadau wengine wakishuhudia yaliyokuwa yakijiri ukumbini humo wakati wa uzinduzi wa albamu mpya ya Rose Muhando iliyojulikana kwa jina la Shikilia Pindo la Yesu.


Sehemu ya umati wa watu waliohudhuria onesho hilo.

Washabi na wapenzi wa muziki wa injili wakiendelea kushuhudia yaliyokuwa yakijiri kwenye uzinduzi wa albamu ya Rose Muhando.

Palikuwa hapatoshi jukwaani

Mwimbaji John Lissu akiimba sambamba na skwadi lake

Mwenye kuguswa alijikuta akisimama na kuimba

Mwimbaji mahiri wa nyimbo za Injili kutoka nchini Zambia Ephraim Sekelet akiimba mbele washabi na wapenzi wa muziki huo,waliokuwa wamefurika ukumbini humo.

Rose Muhando akiimba sambamba washabiki wake jukwaani

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog