Hatima yake shakani: Bado dili la Man United kuendelea kumsajili Arturo Vidal linaendelea.
UHAMISHO wa Arturo Vidal kutoka klabu ya
Juventus kwenda Manchester United umeingia shakani kwa sababu nyota
huyo wa Chile hayupo fiti, hii ni kwa mujibu wa kocha wa timu ya taifa
ya Chile.
Jorge Sampaoli, alikaririwa huko El Mercurio,
akisema bosi wa Man United, Louis Van Gaal anaogopa kutumia paundi
milioni 47 kumsajili kwasababu kiungo huyo ana matatizo ya goti.
Vidal kwa muda mrefu amekuwa akiwaniwa
na Man United na ripoti zinasema kuwa dili hilo linakaribia kukamilika
majira haya ya kiangazi.
Hayupo fiti: Bosi wa Chile, Jorge Sampaoli anasema Louis van Gaal anaogopa kumsajili Vidal kwasababu ya majeruhi.
'Najua tatizo kubwa katika uhamisho wa
Vidali wa dola za kimarekani milioni 80 (paundi milioni 47) kutoka
Juventus kwenda Man United, ni Louis van Gaal kuwa na wasiwasi wa
kuimarika kwa goti la Vidal,' Sampaoli aliliambia gazeti la Chile.
Vidal alifanyiwa upasuaji wa goti mwezi
mei mwaka huu na aliharakishwa kupata matibabu ili kucheza fainali za
kombe la dunia majira ya kiangazi mwaka huu nchini Brazil.
0 maoni:
Post a Comment