FRANK James Lampard, mwenye miaka 36, mpaka sasa amecheza
mechi 973 kwa klabu na nchi yake katika maisha ya soka.
Anahitaji mechi 27 tu kufika digiti nne na kitu
hicho anaweza kufanya kupitia michuano ya ligi kuu soka nchini England baada ya
kujiunga na Manchester City kwa mkopo kutoka klabu ya New York City mwezi huu.
Kiungo huyo mkongwe ataitumikia Man City mpaka mwezi
Januari mwakani ambapo ataende NYCFC kujiandaa na michuano ya ligi kuu nchini
Marekani.
Atakuwepo kwa michezo 23 ya ligi kuu, mechi sita
za ligi ya mabingwa, ataanza kombe la Capital One na FA na mechi ya Ngao ya
Hisani itakayopigwa siku ya jumapili.
Lampard ambaye bado hajastaafu soka la kimataifa,
ana nafasi kubwa ya kuongeza mechi zake 106 alizocheza kwa timu ya taifa baada
ya kurudi ligi kuu.
Lampard ndiye mchezaji aliyecheza mechi nyingi
zaidi kwa taifa lake. Pia alicheza England B na alicheza mara 19 katika timu ya
taifa ya vijana chini ya miaka 19.
Kiungo huyo alicheza mechi 187 akiwa na Westaham,
klabu yake ya kwanza na alicheza mechi 11 akiwa kwa mkopo Swansea kabla ya
kwenda kucheza mechi 649 katika miaka 13 aliyocheza Chelsea, na kujiweka katika
nafasi ya tatu ya kucheza mechi nyingi klabuni hapo nyuma ya Peter Bonetti na
mchezaji anayeshikilia rekodi Ron Harris.
Mchezaji wa mwisho wa England kufikisha mechi
1,000 katika timu ya wakubwa alikuwa kocha msaidizi wa Manchester United, Ryan
Giggs ambapo alifikisha idadi hiyo mwaka 2013 kwenye mechi za ligi ya mabingwa
dhidi ya Real Madrid.
Kocha wa sasa wa Fleetwood, Graham Alexander, ambaye aliichezea Scunthorpe United, Luton Town, Preston North End na Burnley alifikisha mechi 1,00 mwezi aprili 2011.
0 maoni:
Post a Comment