Klabu
ya Inter Milan imetoa ofa ya paundi mil 20 kwa Chelsea ili kumsajili
mshambuliaji wake mkongwe Fernando Torres. Milan wamefikia uamuzi huu
baada ya maneno ya Mourinho aliyoyatoa wiki mbili zilizopita kuwa
anahitaji kusajili mshambuliaji mpya kutokana na ubutu wa washambualiaji
alionao. Kutokana na kauli hii ya Mourinho mshambualiji huyu amekuwa
hana raha ikizingatiwa kuwa Eto'o ndiye anapewa nafasi zaidi kwenye
mechi nyingi kubwa. Uwezekano wa mchezaji huyu kwenda Inter Milan msimu
ujao ni mkubwa kutokana na mipango mikubwa ya klabu hii kutaka
kujiimarisha na kurudisha jina lake. Inter Milan tayari imeshamsajili
Nemanja Vidic na itaendelea kutafuta wachezaji wengine wenye majina.
0 maoni:
Post a Comment