Saturday, March 8, 2014


Manchester United wanapata bao kupitia kwa Phil Jones bao la kichwa baada ya Robin Van Persie kuachia shuti kali la frii kiki, Katika dakika ya 34. Phil Jones likiwa ni bao lake la tatu kwa msimu huu. Kipindi cha kwanza Man United wanaenda mapumziko wakiwa mbele ya bao 1-0 dhidi ya wenyeji West Brom. Kipindi cha pili dakika ya 63 United wanafanya mabadiliko Robin van Persie anatoka na nafasi yake inachukuliwa na Danny Welbeck. Kipindi cha pili United wanaongeza bidii na kasi na hatimae dakika ya 65 Wayne Rooney anaipachikia bao la pili na kufanya 2-0 bao la kichwa baada ya mpira kupigwa kama kona na Rafael na Rooney kujitwisha mpira huo kiurahisi mpaka langoni mwa timu ya West Brom Albion. Dakika za mwishoni dakika ya 82 Mchezaji wa United aliyetokea benchi na kuchukua nafasi ya Van Persie Danny Welbeck akaiongezea bao la tatu United kwa kufanya 3-0 baada ya kutanguliziwa pasi safi na Wayne Rooney.
Kocha wa Man United David Moyes akiingia uwanjani Hawthorns.
Mashetani wekundu wakipongezana 
Kushinda ni raha!! David MoyesRooney akichuana na mchezaji wa West Brom Gareth
Januzaji akifanya mambo yake...Wayne Rooney akifunga bapo la kichwa kipindi cha pili...
VIKOSI:
West Brom: West Brom: Foster; Reid, McAuley, Olsson, Ridgewell; Yacob, Mulumbu; Amalfitano, Gera, Brunt, Anichebe
Substitutes: Morrison, Myhill, Vydra, Dawson, Sessegnon, Berahino, Koulossa
Manchester United: De Gea; Rafael, Jones, Smalling, Evra; Carrick, Fellaini; Mata, Rooney, Januzaj; van Persie
Substitutes: Giggs, Lindegaard, Vidic, Young, Welbeck, Fletcher, Kagawa

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog