Jumla
ya wachezaji watatu wametajwa kwenye orodha ya wachezaji ambao wapo
kwenye rada ya Barcelona kusajiliwa mwishoni mwa msimu. Wachezaji hao ni
David Luiz (chelsea), Jan Vertonghen (spurs) na Mats Hummels
(Dortmund). Kati ya wachezaji hawa mmoja ndiye atakayeweza kusajiliwa na
Barcelona ili kuziba pengo la Carles Puyol ambaye ameshatangaza
kuondoka Barca kutokana na kuwa majeruhi muda mrefu. Mwishoni mwa mwaka
jana Barcelona ilikuwa na nia ya kumsajili Luiz, lakini Mourinho aliweka
ngumu hivyo usajili huu ulishindikana. Jambo hili linategemewa kutokea
tena mwishoni mwa msimu huu kwani Mourinho na Barcelona ni maadui wa
damu. Kutokana na hali hii, Barcelona wana nafasi kubwa kuwasajili
Vertonghen na Hummels kuliko Luiz.
0 maoni:
Post a Comment