Wang’amuzi
vipaji 28 wanakutana Lushoto mkoani Tanga kwa siku saba katika mpango
maalumu wa maboresho ya Taifa Stars ambapo watatoka na orodha ya mwisho
ya wachezaji waliopatikana katika mechi za maboresho hayo zilizochezwa
nchi nzima.
Katika
kikao hicho, wang’amuzi hao watapitia majina ya wachezaji walioteuliwa
ikiwemo kuwaangalia tena kwenye video kwa vile mechi zote zilirekodiwa.
Wachezaji watakaoteuliwa katika mpango huo baadaye wataingia kambini
mkoani Mbeya.
Wang’amuzi
vipaji ambao wanaoondoka Machi 9 mwaka huu kwenda Lushoto ni Abdul
Mingange, Boniface Pawasa, Charles Mkwassa, Dan Korosso, Dk. Mshindo
Msolla, Edward Hiza, Elly Mzozo, Hafidh Badru, Hamimu Mawazo, John
Simkoko, Jonas Tiboroha, Juma Mgunda na Juma Mwambusi.
Kanali
mstaafu Idd Kipingu, Kenny Mwaisabula, Madaraka Bendera, Madaraka
Selemani, Mbarouk Nyenga, Mohamed Ally, Mussa Kissoky, Nicholas Mihayo,
Peter Mhina, Salum Mayanga, Salvatory Edward, Sebastian Nkoma, Sekilojo
Chambua, Selemani Jabir na Shabani Ramadhan.
Wengine
ni Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF ambaye pia ni Mwenyekiti wa
Kamati ya Ufundi, Kidao Wilfred, Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF
ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Vijana, Ayoub Nyenzi, Kaimu
Mkurugenzi wa Ufundi, Salum Madadi na Mshauri wa Rais (Ufundi),
Pelegrinius Rutayuga.
0 maoni:
Post a Comment