Thursday, July 17, 2014


Official: Rio Ferdinand joins QPR on one-year deal
Imechapisha Julai 18, 2014, saa 1:00 asubuhi

NAHODHA wa zamani wa Manchester United na England, Rio Ferdinand amesaini mkataba wa mwaka mmoja katika klabu ya QPR, klabu hiyo mpya iliyopanda daraja imethibitisha.
Mtandao wa Goal.com uliripoti mwezi juni mwaka huu kuwa klabu hiyo iliyopanda ligi kuu ilikuwa na nia ya kumsaini Ferdinand baada ya kumaliza mkataba na klabu yake ya Man United.
Ferdinand alithibitisha kuondoka Old Trafford mwezi mei mwaka huu baada ya kuitumikia timu hiyo kwa miaka 12 ambapo alicheza mechi 454 na alishinda makombe sita ya ligi kuu na ligi ya mabingwa (UEFA) mwaka 2008.
“QPR ni klabu ya kwanza inayocheza ligi  kunisajili mimi. Ni kumbukumbu kubwa kwangu-na kwa familia yangu,” aliuambia mtandao wa klabu hiyo.
“Nilizungumza kwa kirefu na Harry na (mwenyekiti) Mr (Tony) Fernandes. Nadhani wote walionekana kunikubali na wakaona bado kuna kitu naweza kufanya-hiyo ndio ilinifanya niwe na hamu ya kuja hapa na kucheza mpira”.

“Nilikuwa na ofa nyingi duniani kote-baadhi ya sehemu zilikuwa nzuri kuliko hapa. Lakini malengo yangu yalikuwa kucheza ligi kuu ya England na kurudi hapa ambapo ilianzia”.

Harry Redknapp alifanya kazi na Ferdinand wakati beki huyo alikuwa kijana mdogo katika klabu ya West Ham na kocha huyo wa QPR imefurahi kuungana tena na mkongwe huyo.
“Nimefurahi sana,” aliongeza. “Rio ni mchezaji mkubwa na waajabu.
Nimefurahi kwasababu tumeweza kumleta hapa”.
“Nilimsajili Rio akiwa na miaka 14. Muda wote akiwa ndani na nje ya uwanja alipenda kujifunza, ameendelea kufanya hivyo katika maisha yake yote ya mpira”.

“Wakati anacheza Manchester United,  alikuwa ndiye beki bora barani Ulaya, kama sio dunia nzima”.

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog