Tangazo rasmi: Arsenal walitangaza hadharani usajili huo kupitia mtandao wake wa Twita ambapo waliweka picha na ujumbe.
Imechapishwa Julai 18, 2014, saa 1:45 asubuhi
KLABU ya Arsenal imemsajili beki wa kulia wa Ufaransa Mathieu Debuchy kutokea klabu ya Newcastle.
Debuchy, mwenye miaka 28, amesajiliwa kwa nia ya kuziba pengo la beki wa kulia, Mfaransa mwenzake, Bacary Sagna aliyetimka Emirates na kujiunga na mabingwa wa ligi kuu, Manchester City majira haya ya kiangazi mwaka huu.
Asernal alitweet picha ya Debuchy ikisindikizwa na ujumbe uliosomeka #Karibu Debuchy.
Jembe jipya: Debuchy aliichezea Ufaransa mechi nne kati ya tano za kombe la dunia nchini Brazil na alionesha kiwango cha juu.
Karibu: Pia Arsenal iliposti picha ya jezi ya mfaransa huyo kwenye mtandao wake rasmi wa Instragram.
Debuchy alijivunia usajili huo na akasisitiza kuwa umuhimu wa ligi ya mabingwa ndio kichocheo cha yeye kujiunga na Asernal.
"Najivunia kujiunga na klabu kubwa kama
hii na kuvaa rangi zake, ni moja ya klabu kubwa zaidi duniani," beki
huyo wa kulia aliuambia mtandao wa Asernal.com.
"Naangalia mbele nikiwa na Aserne Wenger na kuisaidia timu kuendeleza mafanikio ya msimu uliopita ya kutwaa kombe la FA".
"Kucheza tena ligi ya mabingwa ni
fuaraha kubwa kwangu na nitajitahidi kadiri ya uwezo wangu kuisaidia
Asernal kushindania kombe"
Debuchy amewasili Arsenal kurithi
mikoba ya Bacary Sagna ambaye hakuonesha kiwango kikubwa katika fainali
za kombe la dunia akiwa na Ufaransa.
Pozi bab kubwa!: Debuchy alisema amefurahi kucheza ligi ya mabingwa tena.
Ametokelezea: Nyota huyu atakuwa chaguo
la kwanza katika nafasi ya beki wa kulia baada ya kuondoka kwa Sagna
aliyejiunga na Manchester City
Karibu: Arsene Wenger aliweka wazi kuwa uzoezi mkubwa wa Debuchy ndio sababu ya msingi ya kumleta kikosini beki huyo Mfaransa
0 maoni:
Post a Comment