Anaenda Magharibi: Rio Ferdinand anatarajia kujiunga na QPR baada ya kuondoka Manchester United.
Imechapishwa Julai 17, 2014, saa 6:46 mchana
BEKI mkongwe, Rio Ferdinand hatarithi mikoba ya unahodha wa Clint Hill katika klabu ya QPR mara atakapokamilisha uhamisho wake.
Ferdinand anamalizia taratibu za
kujiunga na klabu hiyo ya Magharibi mwa London na anatarajiwa kusaini
mkata muda wowote kutoka sasa.
Nahodha huyo wa zamani wa Manchester
United na timu ya Taifa ya England yupo katika hatua ya mwisho ya
makubaliano ya mkataba mwa mwaka mmoja na QPR baada ya kuondoka Old
Trafford mwishoni mwa msimu uliopita.
Ukurasa mpya: Ferdinand anataka kujiuna na QPR
Uhamisho huo utamkutanisha na kocha
Harry Redknapp, ambaye alimsajili kwa mara ya kwanza akiwa mdogo katika
klabu ya West Ham miaka 21 iliyopita.
Redknapp alisema:"Ni dili kubwa. Rio atakuwa mchezaji mkubwa kwetu kutokana na maarifa na uzoefu wake katika mchezo wa soka".
Licha ya uzoefu wake uwanjani, Redknapp hatampa unahodha klabuni hapo.
0 maoni:
Post a Comment