Thursday, July 17, 2014


Imechapishwa Julai 17, 2014, saa 8:23 mchana

Timu ya Azam Fc leo imepata ushindi wa magoli mawili kwa moja Dhidi ya Jkt Ruvu katika mchezo wa kirafiki uliochezwa kwenye Uwanja wa chamazi Complex uliopo chamazi.
Azam ndio walioanza kufunga magoli hayo kupitia kwa Kavumbagu na Kipre Tchetche kipindi cha kwanza wakati bao la JKT ruvu likifungwa na Ally Bilali.
Katika Mchezo huo Kocha wa Azam Fc Joseph Omog aliwatumia wachezaji wa timu ya Vijana ya Azam kuangalia viwango vyao.
Kocha Omog bado amesema anahitaji mechi za kirafiki zaidi ili kukitengeneza kikosi chake huku akiwasubili wachezaji waliopo kwenye majukumu ya timu ya tafa.
Wachezaji wa Azam Fc waliopo kwenye Timu ya Taifa ni Tisa ambao ni Aishi Manula, Agrey Moris, Shomari Kapombe, Saidi Morad, Erasto Nyoni, Himid Mao, Mcha Hamis, Kelvin Friday pamoja na John Bocco

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog