Na Boniface Wambura, Dar es salaam
Timu
ya Taifa ya Msumbiji (Mambas) inawasili Dar es Salaam kesho (Julai 18
mwaka huu) kwa ajili ya mechi ya michuano ya Afrika dhidi ya Taifa Stars
itakayochezwa Jumapili, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Mambas
itatua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) saa 7.30
mchana kwa ndege ya LAM ikiwa na msafara wa watu 37 ambapo kati ya hao,
25 ni wachezaji.
Wachezaji
kwenye msafara huo ni Almiro Lobo, Apson Manjate, Bone Mario Uaferro,
Dario Ivan Khan, Edson Sitoe, Eduardo Jumisse, Gelicio Aurelio Banze,
Helder Pelembe, Josemar Machaisse, Elias Pelembe, Isac Carvalho na
Jeffrey Constatino.
Wengine
ni Manuel Fernandes, Manuel Uetimane, Mario Sinamunda, Momed Hagi,
Reginaldo Fait, Reinoldo Mandava, Ricardo Campos, Saddan Guambe, Simao
Mate Junior, Soares Victor Soares, Stelio Ernesto, Vando Justino na
Zainadine Junior.
Timu
hiyo itafikia kwenye hoteli ya Accomondia, na itaondoka Jumapili mara
baada ya kumalizika kwa mechi hiyo itakayochezeshwa na mwamuzi Mahmoud
Ashour.
0 maoni:
Post a Comment