Thursday, July 17, 2014


Staying put: Louis van Gaal says he will find roles for Paul Scholes and Phil Neville
Mtabakia: Louis van Gaal amesema atawatafutia kazi Paul Scholes na Phil Neville.

Imechapishwa Julai 17, 2014, saa 12:36 jioni

LOUIS van Gaal ameahidi kuwajumuisha Paul Scholes na Phil Neville katika benchi la ufundi la Manchester United.
Mholanzi huyo aliyeanza kazi rasmi United wiki hii amesema atawatafutia kazi ya kufanya katika benchi lake.
Ryan Goggs tayari alishateuliwa kuwa msaidizi wa pili wa Van Gaal na Nicky Butt alibaki kuwa kocha wa timu za vijana.
Kocha huyo wa zamani wa Uholanzi amethibitisha kuwa Neville na Scholes ambao kwa pamoja walikuwa wachezaji wa kikosi cha mwaka 1992 kilichoshinda kombe la FA, watapatiwa kibarua cha kufanya.
Alisema: "Nicky Butt tayari anatusaidia. Tutatafuta kazi ya Paul Scholes na Phil Neville. Hicho ndicho tunataka".
"Tunatakiwa kurithi ubora wa watu hawa na tutazungumza na kila mtu binafsi na tusubiri na kuona"
The new team: Van Gaal will be assisted by Ryan Giggs
Timu mpya: Van Gaal atasaidiwa na Ryan Giggs
Getting his points across: Van Gaal speaks to the media for the first time as Manchester United manager
Van Gaal akizungumza na waandishi wa habari kwa mara ya kwanza katika klabu ya  Manchester United.

Neville aliletwa Old Trafford na kocha aliyefukuzwa kazi, David Moyes kama msaidizi wake wa timu ya kwanza na alibakishwa baada ya Giggs kuteuliwa kuiongoza Man United kwa muda katika mechi nne za mwisho za msimu uliopita.
Inafahamika kuwa United walitaka kumbakisha Neville kwa pointi kuwa mchezaji huyo wa kikosi cha 1992 ni muhimu katika klabu hiyo, lakini kutokana na ujio wa Van Gaal majukumu ya kocha huyo yanaweza kupunguzwa zaidi ukilinganisha na msimu uliopita.

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog