Mjumbe
wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF),
Lina Kessy ameteuliwa kuwa Ofisa Michezo wa Umoja wa Afrika (AU).
Uteuzi
huo umefanywa na Mwenyekiti wa Kamisheni ya AU, Nkozasana Dlamini-Zuma,
na Lina atatumikia nafasi hiyo kwa mkataba wa miaka mitatu katika makao
makuu ya AU yaliyopo Addis Ababa, Ethiopia.
Lina
ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu wa Wanawake
Tanzania (TWFA) amewashukuru wote ambao kwa michango yao ya hali na mali
imemwezesha kufika hapo.
Ameishukuru
TFF kwa kumlea na kumjenga. Shukrani nyingine amezitoa kwa Serikali
kupitia Kurugenzi ya Michezo, Baraza la Michezo la Taifa (BMT) na Kamati
ya Olimpiki Tanzania (TOC).
TFF
inampongeza kwa uteuzi huo, na tunaamini ataipeperusha vyema bendera ya
Tanzania ikiwemo kuwa chachu ya maendeleo ya michezo kwa Tanzania na
Afrika kwa ujumla.
BONIFACE WAMBURA
OFISA HABARI NA MAWASILIANO
SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
0 maoni:
Post a Comment