Bosi mpya: Louis van Gaal alifanya mkutano wake wa kwanza na waandishi wa habari leo tangu ajiunge na Manchester United.
LOUIS van Gaal amesema
Manchester United ni klabu kubwa duniani, lakini inatakiwa kujijenga
upya baada ya kuvurunda msimu uliopita.
Van Gaal amefanya mkutano wake
wa kwanza na waandishi wa habari tangu ajiunge na Man United baada ya
kumaliza nafasi ya tatu ya kombe la dunia akiwa na timu ya Taifa ya
Uholanzi.
Mholanzi huyo ameisifu klabu ya
United kuwa ni kubwa katika ulimwengu wa soka, lakini aliwakumbuksha
mashabiki kuwa maboresho ya haraka yanahitajika ili kuepukana na majanga
waliyokumbana nayo msimu uliopita.
Gwiji wa zamani na gwiji ajaye? Louis van Gaal akitambulishwa kwa waandishi wa habari na Sir Bobby Charlton.
“Msimu uliopita mlikuwa wa saba, kwahiyo ninyi sio klabu kubwa. Mnatakiwa kujithibitsha wenyewe,” alisema.
0 maoni:
Post a Comment