Meneja
wa Kilimanjaro Premium Lager, George Kavishe akimkabidhi vifaa Makamu
wa Rais wa Simba SC, Geoffrey Nyange. (Picha: Executive Solutions).
Meneja
wa Kilimanjaro Premium Lager, George Kavishe akimkabidhi vifaa
Mkurugenzi wa Masoko wa Yanga, George Simba. Anayeshuhudia ni Hafidh
Saleh, Meneja wa Yanga. (Picha: Executive Solutions).
Meneja
wa Kilimanjaro Premium Lager, George Kavishe akiwakabidhi vifaa Makamu
wa Rais wa Simba SC, Geoffrey Nyange pamoja na Mkurugenzi wa Masoko wa
Yanga George Simba (Picha: Executive Solutions).
Ikiwa ni sehemu ya udhamini
wake, bia ya Kilimanjaro Premium Lager imekabidhi vifaa vya michezo kwa
klabu maarufu za Simba SC na Young Africans SC kwa ajili ya msimu wa
2014/15 wa Ligi Kuu inayotarajiwa kuanza mwezi ujao. Meneja wa bia ya
Kilimanjaro Premium Lager, George Kavishe alisema “Tunawapatia vifaa
mapema kabla ya ligi kuanza ili wapate muda wa kutosha kujiandaa kwa
ajili ya msimu wa 2014/15 ambayo bila shaka itakuwa na changamoto kubwa
kwa timu hizi mbili na pia tunaamini kuwa siri ya mafanikio katika
michezo ni maandalizi mazuri. Ni matumaini yetu kuwa wachezaji wapya
waliosajiliwa Simba na Yanga wataiwakilisha Kili vizuri na kufurahia
kuzichezea klabu hizi kongwe.” Kavishe aliongeza kuwa Vifaa ambavyo leo
tunatoa ni pamoja na mipira, viatu, soksi, shin guards, nguo za mazoezi,
nguo za kawaida, gloves na vitu vingine vingi ambavyo vitawezesha timu
hizi za Simba na Yanga kucheza wakifurahia kuvaa vifaa vyenye ubora wa
hali ya juu. Kilimanjaro Premium Lager kama mdhamini mkuu wa Simba na
Yanga, na kinywaji kinachoongoza katika udhamini wa soka hapa nchini
tunadhani kwamba uhusiano wetu na klabu hizi ni kiungo muhimu sana
katika kuendeleza mpira wa miguu hapa Tanzania. Tutaendelea kutimiza
wajibu wetu kwa klabu hizi na kama ilvyo kawaida yetu, tutahakikisha
tunalifikisha soka la Tanzania kwenye kilele cha mafanikio. Kavishe
alisema kuwa udhamini wa Kilimanjaro Premium Lager kwa Simba na Yanga
umelenga kukuza soka la Tanzania, kuleta msisimko, na kuvutia mashabiki
wengi wa mpira wakati na vilevile kuwaweka wachezaji wa Tanzania katika
nafasi nzuri ya kimataifa. Tunawashukuru viongozi wa Simba na Yanga,
mashabiki wote, vyombo vya habari na wadau wote wa mpira kwa ushirikiano
mzuri tunaoendelea kupata kwenye udhamini wetu na hiyo ndio siri ya
mafanikio ya uhusiano wetu na klabu hizi mbili maarufu. “Tunawaomba
mashabiki wa Simba na Yanga waendelee kuiunga mkono bia yao ya
Kilimanjaro Premium Lager kwani tunafanya kila jitihada kuwapa burudani
na kufikisha soka la Tanzania kwenye kilele cha mafanikio.”
0 maoni:
Post a Comment