Thursday, July 17, 2014


Spanish fly guy: Ander Herrera became Louis van Gaal's first signing in a £28.4m deal
 Ander Herrera alikuwa mchezaji wa kwanza kusajiliwa na  Louis van Gaal kwa dau la puandi milioni 28.4

Imechapishwa Julai 17, 2014, saa 5:27 asubuhi

Nicky Butt amemtabiria Ander Herrera kupata mafanikio katika klabu ya  Manchester United, lakini amekiri kuwa Mhispania huyo hawezi kuwa katika kiwango kimoja na wachezaji kama Toni Kroos au Paul Pogba.
Nyota huyo mwenye miaka 24 alikuwa wa kwanza kusajiliwa majira haya ya kiangazi na kocha mpya wa Manchester United,  Louis van Gaal kutokea klabu ya Atletico Madrid kwa dau la paundi milioni 28.4 .
Wakat huo huo, mchezaji aliyekuwa akiwindwa na Manchester United, Kroos yupo katika hatua za mwisho kukamilisha uhamisho wake kujiunga na Real Madrid.
Naye mchezaji aliyeibukia kutoka akademi ya Man United, Pogba amewekewa ngumu kutoka Juventus ambapo imekaririwa kuwa kama timu inataka saini yake lazima iguse mfuko na kulipa dau nono la paundi milioni 60.
German engineering: Toni Kroos is close to a move to Real Madrid
Herera hawezi kuwa katika kiwango cha Toni Kroos4
French fancy: Paul Pogba has been valued at £60m by Juventus
 Ander Herrera hawezi kuwa katika  kiwango sawa na  Paul Pogba.

Butt, ambaye kwasasa ni miongoni mwa watu wanaounda benchi la Ufundi la Old Trafford, amekiri kuwa Herera anahitaji muda kufikia kiwango cha wapinzani wake.
"Herera hakuwa katika kiwango kikubwa sana, lakini tulilazimika kumchukua kwasababu hakukuwepo na viungo wa kiwango cha juu zaidi,". Alisema Butt.

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog