Thursday, August 21, 2014

Bondia Mohamed Matumla kushoto na Nassibu Ramadhani wakitunishiana misuli 
Na Mwandishi Wetu
MABONDIA Nassibu Ramadhani pamoja na Mohamed Matumla wameingia makubaliano ya kuzipiga kwa mara ya pili siku ya septemba 27 katika ukumbi wa Friends Corner Hotel Manzese Dar es salaam Akizungumzia mpambano huo mratibu wake Yassin Abdallah ‘Ostaadhi’ amesema mabondia hao wamekubaliana na kusaini mkataba wa kuzipiga siku hiyo
 mabondia hao walikutana kwa  mara ya kwanza na bondia Mohamed Matumla alimshinda kwa pointi Nassibu Ramadhani hivyo kuufanya mchezo huu kuwa mgumu zaidi kwa Matumla ili kuendeleza kipigo au Ramadhani kulipiza kisasi
hiyo Septemba 27 Mapambano  ya utangulizi yatakuwa hivi bondia Issa Omari atamkabili juma fundi.Kg 53 raundi nane. na Sadiq Momba vs Tasha Mjuaji Kg 59 raundi nane. wakati Juma Mustafa atamkabili Bakari Dunda Kg 61 raundi sita. huku kina dada Lulu Kayage akipambana na Fatma Yazidu.Kg 51 raundi nne. siku hiyo pia kutakuwa na uuzwaji wa DVD ambazo zinatoa mwanga kwa mchezaji kujua mchezo na kufahamu zaidi mbinu mpya zitumiwazo na mataifa mbali mbali Duniani.
Wakiwemo mabondia bingwa wa dunia kama Manny Paquaio,Floyd Maywether,Amir Khani, Mohamed Ali ,Mike Tayson na wengine wengi wanaotamba na waliotamba katika mchezo  wa masumbwi Duniani

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog