Thursday, August 21, 2014


New boy: Leroy Fer shows off his No 10 QPR shirt after joining the club from Championship side Norwich
Kijana mpya: Leroy Fer akionesha jezi yake namba 10 atakayovaa  QPR .

KIUNGO wa Kiholanzi, Leroy Fer amekamilisha usajili wake wa kujiunga na QPR akitokea klabu inayocheza Championship, Norwich.
Nyota huyo mwenye miaka 24 ambaye amesajiliwa kwa ada ya uhamisho ya paundi milioni 7, amesaini mkataba wa miaka mitatu na kikosi cha kocha Harry Redknapp.
Fer amecheza kwa msimu mmoja katika dimba la Carrow Road baada ya kujiunga na timu hiyo kutokea timu ya Eredivisie ya  FC Twente msimu uliopita.
Fresh start: Fer seals his move to London while sat alongside his wife Xenia Schipaanboord
Nyota kinda: Fer akisaini mkataba wake, pembeni yake ni mke wake  Xenia Schipaanboord

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog