Thursday, August 21, 2014


How it's going to be: Mario Balotelli mocked up in a Liverpool shirt in anticipation of his £16m move to Anfield
Anaenda kuwa hivi: Mario Balotelli ametengenezwa akiwa amevalia jezi ya Liverpool.

LIVERPOOL wamekubali kuilipa AC Milani ada ya uhamisho ya paundi milioni 16 ili kuinasa saini ya mshambiliaji wa Italia, Mario Balotelli.
Mwezi uliopita, Brendan Rodgers alisema Liverpool haiwezi kumsajili Balotelli, lakini amebadili moyo wake.
Mapema leo Balotelli aliwaambia Sky Italia: "Leo itakuwa siku yangu ya mwisho Milanello."
Super Mario: Balotelli left the Premier League in 2013, but now seems to be on his way back with Liverpool
Super Mario: Balotelli aliondoka ligi kuu nchini England mwaka 2013, lakini yuko njiani kurudi na safari hii anatua Liverpool 
Change of heart: Rodgers had previously said he would not be signing the Italian striker
Amebadili moyo: Rodgers awali alikataa kumsajili mshambuliaji huyo wa Italia.
Stats: Balotelli's Premier League record (via Opta)
Stats: Balotelli's Premier League record (via Opta)

Nyota huyo kurudi England kutateka hisia za mashabiki wengi wa soka wakikumbuka vituko vyake akiwa Manchester City kabla ya kuondoka mwaka 2013.
Balotelli amejihusisha na matukio mengi ya utovu wa nidhamu hususani wakati akicheza ligi kuu England 
Ndani ya uwanja, alioneshwa kadi nyekundu wakati Man City ilipochuana na Asernal mwaka 2012 na kufungwa.
Nje ya uwanja, alikuwa na matukio ya mengi ya ukutuku.
Moja ya tukio la kukumbukwa pia ni kitendo chake cha kuonesha fulana iliyoandikwa 'Why Always Me?' alipofunga goli kwenye mechi ya mahasimu wa Manchester ndani ya dimba la Old Trafford mwaka 2011.
Pia aliingia katika mgogoro na kocha wa City wakati ule, Roberto Mancini ndani ya uwanja wa mazoezi na kukunjana.
Zaidi alimchapa kibao Jerome Boateng.
Tangu aliporudi nchini Italia amefunga mabao 30 katika mechi 54, idadi sawa na aliyofunga akiwa na City katika mechi 80.
Si rahisi kusahau kuwa nyota huyu tayari ameshinda makombe manne katika mataifa mawili, ubingwa ligi na kombe la FA na Coppa Italia akiwa na umri wa miaka 24.

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog