Thursday, March 13, 2014

_MG_0354

WAKATI zoezi la upigaji kura kuchagua, mgeni rasmi, waimbaji na mikoa itakayofanyika tamasha la Pasaka mwaka huu, baadhi ya mameneja  wa viwanja vya michezo hapa nchini wamelizungumzia tamasha hilo kwamba ingekuwa vema lingefanyika kwenye mikoa yao.
Kwa kutambua umuhimu wa waumini,  mashabiki na wadau wa nyimbo za Injili hapa nchini, Kampuni ya Msama Promotions kupitia Mkurugenzi wake, Alex Msama imeyakabidhi masuala hayo mikononi mwa wadau hao ambao ndio watachagua wanachokitaka katika tamasha hilo la kumuimbia na kumtukuza Mungu kupitia waimbaji mbalimbali.
Msama amendelea kuwakumbusha watanzania namna ya kuwapigia kura waimbaji, mgeni rasmi na mikoa ambako ukitaka kumpigia mwimbaji andika Pasaka acha nafasi kisha andika jina la mwimbaji unatuma kwenda namba 15327.
Pia kwa mgeni rasmi  andika neno Pasaka acha nafasi kisha andika jina la mgeni rasmi unayetaka kumpigia kura tuma kwenda15327, wakati mikoa unaandika Pasaka acha nafasi jina la mkoa unaotaka kuupigia kura tuma kwenda namba 15327 piga kura uwezavyo ili upate mwimbaji na mgeni rasmi na mkoa unaopenda tamasha lifanyike.
Aidha Msama alitoa wito kwa mashabiki kupiga kura kwa wingi kuchagua maeneo hayo matatu yatakayofanikisha tamasha hilo, kwani litafanikiwa baada ya wao kufanya hivyo.
Meneja wa uwanja wa Majimaji, ambaye ni Katibu Msaidizi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Ruvuma, Nebret Mwinisongole anasema Pasaka ni sikukuu ambayo inaelezea jinsi mkombozi wetu Yesu Kristo alivyoshinda mateso na kueleza kwamba tuendelee kuwa na imani naye kupitia sikukuu hiyo.
Mwinisongole anasema Watanzania  waendelee kudumisha amani ya nchi ambayo tumepewa na Mungu ambayo inatakiwa idumishwe zaidi na viongozi waliopo.
Katibu huyo alifika mbali zaidi kwa kueleza kwamba, Mkoa wa Ruvuma ndio mkoa unaoongoza kwa kuzalisha chakula kingi hapa nchini, hivyo kwa neema hiyo wanawakaribisha waimbaji  mbalimbali wa Kimataifa mkoani kwao kujionea vivutio vilivyoko mkoani humo.
“Mashabiki wa muziki wa Injili waje kwa wingi kusikiliza maneno ya Mungu kupitia waimbaji mbalimbali watakaokuwepo kwenye tamasha hilo,” alisema Mwinisongole.      
Meneja wa uwanja wa Samora mkoani Iringa, Lazaro Manila anasema mashabiki wa Mkoa wa Iringa kupiga kura kwa wingi ili mkoa huo upate nafasi ya Tamasha hilo kufanyika mkoani humo.
Manila anasema iwapo, Iringa watapata nafasi ya kuchaguliwa kufanyika kwa tamasha hilo mkoani kwao itasaidia kuongeza chachu ya waimbaji wazawa kuongeza juhudi za kufikia walipo wenzetu waliopiga hatua.
Meneja wa uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, Rich Urio anasema matamasha yanayoandaliwa na Msama Promotions ni bora na ni muhimu  kwa sababu yanazungumzia amani na kuongeza hofu ya Mungu.
Urio anasema mkoa wa Dar es Salaam hasa uwanja wa Taifa ni eneo muhimu ambalo linakusanya idadi kubwa ya waumini, hivyo anatoa wito kwa wakazi wa mkoa huo kupiga kura kwa wingi kuuchagua mkoa huo.
Urio anasema Msama afanikishe tamasha hilo katika mikoa mingi zaidi kwa siku moja Jumapili ya Pasaka kwa sababu ndio siku muhimu duniani.
“Matamasha yanayoandaliwa na Msama Promotions yana mvuto zaidi hasa wanavyowashirikisha waimbaji kutoka nje kama Solly Mahlangu na Ambassodors of Christ  ambao wanafikisha neno la Mungu inavyotakiwa,” alisema Urio.
Urio anasema viingilio vinavyopangwa na kampuni hiyo ni sahihi kwa sababu haviwaumizi waumini wanaohudhuria kwenye matamasha hayo.

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog