Msafara
wa Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara timu ya Young
Africans leo asubuhi umeondoka jijini Dar es salaam kuelekea mjini
Morogoro tayari kwa mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar siku ya jumamosi, mechi
itakayopigwa kwenye dimba la Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
Young
Africans inayonolewa na makocha Hans Van der Pluijm kutoka Uholanzi,
Charles Mkwasa na Juma Pondamali wazawa jana jioni ilifanya mazoezi
katika Uwanja wa Kaunda ikiwa ni masaa 10 baada ya kuwasili kutokea
jijini Cairo ilipocheza dhidi ya Al Ahly katika mashindano ya Klabu
Bingwa barani Afrika.
Kuhusu
mchezo wenyewe Kocha Hans amesema haifahamu vizuri timu ya Mtibwa Sugar
lakini kwa kushirikiana na wenzake wamejiandaa kuhakikisha timu
inafanya vizuri na kupata pointi 3 katika mchezo huo, yaliyotokea Misri
yameshapita sasa kilichobakia ni kutetea Ubingwa wa Ligi Kuu.
0 maoni:
Post a Comment