Kocha wa Simba SC, Mcroatia, Dravko Logarusic akitoa maelekezo kwavijana wake
Na Baraka Mpenja wa Fullshangwe, Dar es salaam
0712461976 au 0764302956
WEKUNDU
wa Msimbazi Simba wamelaumu timu zinazoingia kwa kukamia wapinzani wao
katika mitanange ya lala salama ligi kuu soka Tanzania bara msimu wa
2013/2014.
Akizungumza
na mtandao huu, afisa habari wa Simba Asha Muhaji amesema hali ya
kukamiana uwanjani inaharibu ubora wa mpira katika mechi mbalimbali.
“Kuna
wakati unaweza kushangaa, mchezaji fulani akawa na kazi ya kumkaba kwa
nguvu mshambuliaji wenu. Mfano Amissi Tambwe kwa Simba, badala ya
kucheza mpira kwa ufanisi, yeye anacheza kimabavu na kumjeruhi mwenzake.
Sasa mpira kama huu hauna maana”. Alisema Asha.
0 maoni:
Post a Comment