Rais
wa Shirikisho la soka duniani, FIFA Sepp Blatter, ameelezea wasi wasi
wake kuhusiana na maandamano yanayoendelea nchini Brazil, huku taifa
hilo likijiandaa kuwa mwenyeji wa kombe la dunia. Kwa
mara ya kwanza katika historia ya FIFA, Blatter amesema hakutakuwepo
kwa hotuba wakati wa sherehe za ufunguzi. Katika mahojiano na jarida
moja la Ujerumani, Blatter amesema anatarajia kuwa fainali hizo
zitasaidia kutuliza hali ya kisiasa nchini Brazil. Mwaka uliopita rais
wa Brazil, Dilma Rousseff, alizomewa na mashabiki wa soka wakati wa
sherehe za ufunguzi za kombe la Shirikisho, ambalo hutumiwa na FIFA kama
maandalizi ya mwisho kabla ya kuanza kwa kombe la dunia. Waandamanaji
waliandamana katika barabara za miji mingi kabla na baada ya fainali
hizo za kombe la Shirisho, wakipinga ufisadi na gharama za kuandaa
fainali hizo za dunia.
0 maoni:
Post a Comment