WEKUNDU
wa Msimbazi Simba wamelaumu timu zinazoingia kwa kukamia wapinzani wao
katika mitanange ya lala salama ligi kuu soka Tanzania bara msimu wa
2013/2014.
Akizungumza
na mtandao huu, afisa habari wa Simba Asha Muhaji amesema hali ya
kukamiana uwanjani inaharibu ubora wa mpira katika mechi mbalimbali.
“Kuna
wakati unaweza kushangaa, mchezaji fulani akawa na kazi ya kumkaba kwa
nguvu mshambuliaji wenu. Mfano Amissi Tambwe kwa Simba, badala ya
kucheza mpira kwa ufanisi, yeye anacheza kimabavu na kumjeruhi mwenzake.
Sasa mpira kama huu hauna maana”. Alisema Asha.
Asha
aliongeza kuwa kukamia mechi kwa kucheza mpira mzuri hakuna tatizo
kwani kila timu kwa sasa inahitaji ushindi, lakini kukamiana kwa
kuumizana si jambo zuri.
“Kuna
timu zinahitaji ubingwa au nafasi nzuri za juu, vilevile kuna timu
zinakwepa kushuka daraja. Mazingira haya yameifanya ligi iwe ngumu sana.
Lakini tatizo ni uchezaji wa ubabe kwa baadhi ya timu. Kuumia ni
kawaida katika mpira, lakini kuna mazingira mengine yanatokana na
kukamiana”. Alisema Asha.
0 maoni:
Post a Comment