Robin
van Persie akiwa na kiungo wa Ac Milan, Nigel De Jong wiki hii kwenye
chakula cha jioni. Tetesi zinasema kuwa Ac Milan wanamtaka RVP hivyo
wanamtumia De Jong kumshawishi.
Mshambualiji wa zamani wa Man utd, Eric Cantona akihojiwa na polisi kwa tuhuma za kumshambulia mtu mmoja jijini London.
Cantona akipanda kwenye gari la polisi kuelekea kituoni kwa mahojiano zaidi
Washabiki
wa Man city wakiwa kwenye airport ya Newcastle baada ya kutua kutoka
Barcelona walipokwenda kuangalia mechi dhidi ya FC Barcelona. Ndege
iliyowabeba washabiki hawa ililazimika kutua kwenye uwanja wa ndege wa
Newcastle baada ya uwanja wa ndege wa Manchester kuwa na hali mbaya ya
hewa.
Eto'o akiwa kwenye pozi la furaha baada ya mechi wikiendi iliyopita
Cristiano
Ronaldo amejitolea kulipa matibabu yote ya mtoto Erik Ortiz Cruz mwenye
matatizo ya ubongo. Mtoto huyu anatakiwa kufanyiwa upasuaji utakao
gharimu paundi 50,240 pesa ambazo zilikuwa nyingi kwa wazazi wake,
lakini Ronaldo baada ya kusikia jambo hili aliamua kujitolea.
Erik Ortiz Cruz akiwa na mama yake
David Beckam akiwa anaendesha pikipiki jijini Rio nchini Brazil wakati akifanya tangazo
Daniel
Sturridge akiwa kwenye pozi nyumbani kwake baada ya kutoka mazoezini.
Sturridge anategemewa kuongoza mashambulizi wikiendi hii kwenye game la
Man utd vs Liverpool.
Dylan
Hartley, Rio Ferdinand, Owen Farrell na Michael Carrick akiwa kwenye
picha ya pamoja baada ya England kushinda dhidi ya Wales kwenye rugby
0 maoni:
Post a Comment