Friday, March 14, 2014

 
Uli Hoeness
Mahakama nchini Ujerumani imemhukumu rais wa
 klabu bingwa Ulaya, Bayern Munich, Uli Hoeness, kifungo cha miaka mitatu na miezi sita jela kwa kukwepa kulipa kodi.
Nyota huyo wa zamani mwenye umri wa miaka 62 alikiri kuitapeli mamlaka ya kutoza ushuru ya Ujerumani mamilioni ya Euro huku akiweka akiba ya fedha zake kisiri kwenye akaunti ya benki ya Uswizi.
Licha ya wakili wake kuiomba mahakama kutomwadhibu Bw Hoeness kwa sababu ya kujisalimisha kwake, mahakimu waliafikia kwamba Hoeness hakukiri kikamilifu.
Hapo awali Hoeness alishtakiwa kwa kukwepa kulipa ushuru wa euro milioni 3.5 (£2.9m; $4.9m) lakini baadaye akakiri kuwa hajawahi kulipa milioni nyingine 15.
Hatimaye Alhamisi, korti ilibaini kuwa alikosa kulipa ushuru wa jumla ya euro milioni 27.2.
Upande wa utetezi umesema kwamba utakata rufaa dhidi ya uamuzi huo.
Hata hivyo Hoeness atabakia kuwa huru hadi uamuzi wa mwisho kabisa utakapotolewa.

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog