Sergio
Aguero ndiye mfungaji hodari wa klabu ya Man city, kwenye mchezo wa
kwanza dhidi ya Barcelona hakuweza kucheza kutokana na majeraha ya mguu.
Aguero amerudi dimbani wiki mbili zilizopita akicheza mechi za ligi na
FA cup. Muda aliyopata kwenye mechi hizi hakika ni mazoezi tosha kuweza
kuwakabili Barcelona usiku wa leo. Ubutu wa mabeki wa Barcelona inaweza
kuwa ni njia rahisi kwa Aguero kuiwezesha timu yake kupata magoli na
hata kuweza kusonga mbele katika michuano hii. Mbali ya Aguero, Man city
pia itawategemea Yaya Toure, Nasri na Silva wakiwa kama wachezaji
tegemezi kwenye sehemu ya kiungo, ambapo ni lazima wacheze kwa juhudi na
uwezo wote ili kupunguza umiliki wa mpira wa Barcelona. Mchezo
uliyopita ulikwisha kwa Barcelona kushinda goli 2-0, hivyo ili Man city
wasongembele wanatakiwa kushinda zaidi ya magoli 2.
Kwa
upande wa Barcelona, ingawa ni timu inayoonekana kama inachechemea
kwenye ligi, bado ni timu tishio barani Ulaya na itashuka dimbani usiku
huu ikiwa na machungu ya kufungwa kwenye mechi ya ligi jumamosi
iliyopita. Ni timu chache sana ambazo zimeweza kuifunga Barcelona kwenye
uwanja wake wa nyumbani ikiwa ni jambo ambalo si jepesi kutokana na
umahiri wa wachezaji wake akiwemo Messi, Neymar, Xavi, Cesc na Iniesta.
Mazingira haya yanaifanya Man city kuwa kwenye wakati mgumu sana kufikia
malengo yao ya kufika hatua ya robo fainali. Ili kujua kitakachotokea
usiku wa leo endelea kutembelea Michezoupdates.
0 maoni:
Post a Comment