Thursday, July 31, 2014


Done deal: Lukaku is unveiled at Everton on Wednesday alongside manager Roberto Martinez
Dili limekamilika: Jana jumatano, Lukaku alitambulishwa na  kocha wake wa Everton, Roberto Martinez.
KOCHA wa Chelsea, Jose Mourinho alimpiga dongo  Romelu Lukaku jana usiku baada ya kukamilisha uhamisho wa paundi milioni 28 kujiunga na Everton.
Lukaku alijiunga na Chelsea msimu mitatu iliyopita, lakini alicheza mechi 10 tu za ligi kuu kabla ya kutolewa kwa mkopo katika klabu West Brom na baadaye Everton.

Akizungumza baada ya ushindi wa mabao 3-1 iliopata Chelsea kwenye mechi ya kirafiki dhidi ya  Vitesse Arnhem, Mourinho, alisema nyota huyo mwenye miaka 21 hakuandaliwa kushindania nafasi ya kucheza klabuni.
Smiles better: The Belgian striker expressed his delight at returning to Goodison Park
Tabasamu: Mshambuliaji huyo wa Everton alifurahia kurudi Goodison Park 
Madongo kama kawaida: Mourinho (kulia) akitazama timu yake ya Chelsea iliyoitandika Vitesse  mabao 3-1 jana jumatano.

Alisema: 'Ukweli ni kwamba Romelu alikuwa wazi kwetu kwamba akili yake haikuwa tayari na hakuwa na morali ya kuja kupambana kutafuta namba katika kikosi cha Chelsea".

"Alitaka kuichezea Chelsea, lakini alihitaji kuwa mshambuliaji chaguo la kwanza, kitu ambacho ni kigumu kwa klabu yetu hasa kwa aina ya mchezaji kama yeye. Alipunguza hamu ya kuja kwetu".
Mourinho alisisitiza kuwa hana tatizo na Lukaku: "Kitu cha msingi ni kwamba ana furaha na anafanya kazi vizuri, ni mtoto mzuri na ana namna yake ya kuwaza mambo yake".
"Yote kwa yote, namtakia kila la kheri. Anastahili bahati na kuwa na furaha".

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog