Chelsea imeichapa Vitesse Arnhem ya Uholanzi kwa mabao 3-1 katika mechi ya kirafiki iliyochezwa.
Lakini
mechi hiyo ilikuwa na rekodi kadhaa, mfano Cesc Fabregas akianza
kuifungia Chelsea bao la kwanza katika hayo matatu, mabao mengine
yalifungwa na Mo Salah, Nemanja Matic.
Diego
Costa ambaye alitengeneza mabao yote matatu alitaka kuzichapa uwanjani
na beki wa Vitesse, Guram Kashia akimtuhumu kumchezea rafu mbaya kwa
makusudi.
Mshambuliaji
aliyerejea Chelsea, Didier Drogba aliendelea kubaki kwenye benchi
akishuhudia Chelsea ikiendelea na mechi za kirafiki.
|
0 maoni:
Post a Comment