Mpya: Viongozi wa ligi kuu nchini
England wamethibitisha kutumia dawa ya kutoweka iliyotumika katika
fainali za kombe la dunia nchini Brazil.
DAWA ya kutoweka iliyotumika kuweka
alama ya kuta za ulinzi kwenye michuano ya kombe la dunia itatumika
katika michuano ya ligi kuu soka nchini England msimu ujao.
Dawa hiyo ya kupulizia inayotoweka
haraka itatumiwa na waamuzi ili kuwaweka wachezaji umbali wa mita 10
kutoka kwenye mpira wakati wa upigaji wa mipira iliyokufa.
Hapa mchezaji hana ujanja wa kudanganya
Dawa hii itatumika kwenye mechi ya kufungua msimu wa ligi kuu baina ya Manchester United na Swansea, agosti 16 mwaka huu.
Mwisho hapa, sawa?
0 maoni:
Post a Comment