GWIJI wa Brazil, Ronaldinho ‘Gaucho’ amethibitisha
kuwa ataondoka Atletico Mineiro, lakini hayupo tayari kustaafu soka.
Nyota huyo mwenye miaka 34 alifurahia maisha yake
ya soka kwa kufanya makubwa akiwa na klabu za Paris Saint-Germain, Barcelona na
AC Milan.
Alishinda mechi 99 na kubeba kombe la dunia mwaka
2002 akiwa na timu ya taifa ya Brazil nchini Japan na Korea kusini.
Tangu aondoke San Siro mwaka 2010, mchezaji huyo
mzaliwa wa Porto Alegre alirudi nchini BrazIl, akijiunga na timu ya Flamengo na
baadaye Atletico ambapo alishinda kombe la Copa Libertadores na sasa anaamini
bado anahitaji kucheza soka zaidi.
“Kustaafu kwasasa, haiwezekani,” aliviambia vyombo vya habari.
“Kwa muda huu kaka yangu( wakala Roberto de Assis) anafikiria kila kitu. Kuanzia wiki ijayo, tutazungumzia hatima yangu ya baadaye. Nitatumia siku hizi chache kukaa mbali na mambo yote ya soka na kupumzika. Lakini najua simu yake inapigwa sana”.
0 maoni:
Post a Comment