Thursday, July 31, 2014


Capello to stay on as Russia boss until 2018


LICHA ya kuboronga kombe la dunia majira ya kiangazi mwaka huu nchini Brazil, Fabio Capello ataendelea kuwa kocha wa timu ya taifa ya Urusi mpaka 2018 .
Waziri wa michezo wa nchi hiyo, Vitaly Mutko amemtania kuwa kama atatwaa kombe la dunia lijalo, atazikwa sehemu aliyozikwa mwandishi gwiji, Fyodor Dostoyevsky.
Muitaliano huyo aliiongoza nchi hiyo ya Ulaya mashariki katika mashindano ya kombe la dunia, lakini alitupwa nje hatua ya makundi ambapo alikuwa na timu za Ubelgiji, Korea Kusini na Algeria.
Hata hivyo, Capello ataendelea kuwa kocha mkuu mpaka 2018 wakati ambao Urusi itakuwa mwenyeji wa fainali zijazo za kombe la dunia na Vitaly Mutko anasema anayo nafasi ya kushinda mioyo ya watu wa Urusi.
“Kama tutafanikiwa kwenye mashindano ya mwaka 2018, tutamzika karibu na Dostoyevsky,” aliwaambia waandishi wa habari.
Wakati huo huo, Capello anajiandaa na michuano ya mataifa ya Ulaya mwaka 2016, lakini amekiri kuwa kipaumbele chake ni fainali za kombe la dunia 2018.

“Lengo kubwa ni kombe la dunia, lakini kwanza tunatakiwa kufuzu michuano ya Ulaya mwaka 2016 nchini Ufaransa,” alisema.

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog