Wilfried Zaha na beki wa zamani wa United Nemanja Vidic wakichuana.
WINGA wa Manchester United , Wilfried
Zaha amesema anatarajia kuwa mchezaji wa aina aitakayo Louis Van Gaal
baada ya msimu uliopita kutoswa na aliyekuwa kocha wa timu hiyo David
Moyes.
Zaha alitoshwa na kocha Moyes na kumtoa
kwa mkopo katika klabu ya Cardiff mwezi januari kwa madai kuwa nyota
huyo ana mitazamo mibaya.
Kinda huyo mwenye miaka 21, sasa amepewa
nafasi ya kuonesha uwezo wake kwa Van Gaal na katika mechi ambayo Man
United ilishinda kwa penati dhidi ya Inter Milan, kocha huyo alimwacha
Zaha mpaka kipindi cha pili ili aoneshe ujuzi wake katika mechi yake ya
kwanza ya maandalizi ya kabla ya msimu.
Zaha alipewa nafasi ya kumuonesha uwezo kocha Van Gaal kwenye mechi dhidi ya Inter Milan.
Van Gaal amemuambia Zaha kuwa anatakiwa kujitahidi kuwa mshambuliaji wa kati ili aingie katika mfumo wake wa 3-5-2 msimu ujao.
Zaha alisema: "Nilikuwa nacheza winga, lakini kama kocha anataka nizoee nafasi nyingine, nitafanya,"
"Sio kwamba mimi naweza winga tu, nitacheza nafasi nyingine".
"Nimesikia anataka kuwapa nafasi
wachezaji vijana. Hiki ndicho nilihitaji tangu nimefika hapa. Nataka
kuwa mchezaji wa Man United. Natumaini kupata nafasi msimu ujao".
Sir Alex Ferguson alimnunua Zaha januari mwaka 2013 kutokea klabu ya Crystal Palace.
0 maoni:
Post a Comment