Wednesday, February 12, 2014

 




Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger, anatarajiwa kuwa nyota wake aliyesajiliwa kwa kitita cha pauni milioni 42, atarejelea hali yake ya kawaida na kuonyesha mchezo mzuri, baada ya matokeo mabaya wikendi iliyopita.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25, kutoka Ujerumani, hajafunga bao lolote katika mechi nane zilizopita huku akiwa amechangia kuingizwa kwa magoli mawili pekee katika mechi hizo.
Ozil, ambaye alijiunga na Arsenal, kutoka kwa klabu ya Real Madrid Septemba mwaka uliopita, alianza vyema kwa kufunga magoli manne na kuchangia magoli sita katika mechi zake kwanza kumi na mbili za ligi kuu.
Lakini mcheza kiungo huyo, alishutumiwa vikali kufuatia mchezo aliouonyesha wakati Arsenal ilipolimwa magoli 5-1 na Liverpool, hali iliyomlazimu Wenger kumuondoa kunako dakika ya sitini na moja.
Akiongea kabla ya mechi yao katika Uwanja wa Emirates siku ya Jumatano usiku, Wenger alisema kuwa anadhani David Moyes anaweza kufanikiwa kama kocha wa United ikiwa atapewa muda.
Julai mwaka uliopita, Moyes aliteuliwa kuchukua mahala na Sir Alex Ferguson ambaye alistaafu kama kocha wa Manchester United baada ya kushinda ligi kuu ya Premier mara 13 katika kipindi cha miaka 27, lakini amekuwa na kibarua kigumu kufuata nyayo za Ferguson.
Manchester United inashikilia nafasi ya saba kwenye msururu wa ligi kuu na alama 41 na hata ikishinda mechi yake dhidi ya Arsenal, Vijana hao wa Moyes watasalia katika nafasi hiyo hiyo.

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog