Wednesday, February 12, 2014

Meneja wa Chelsea,Jose Mourinho amedai kuwa ni lazima asubiri kwanza kujua kama timu yake imekosa nafasi muhimu katika sare dhidi ya West Bromwich Albion au imekusanya pointi nyingine muhimu.
Chelsea hawakuwa katika ubora wao mzuri katika uwanja wa Hawthorns jana(Jumanne) licha ya kuwa na nyota kama Oscar, Willian, Eden Hazard na Samuel Eto’o walioanza pamoja.
Goli lao katika sare ya 1-1 dhidi ya West Brom inayohaha sana kwasasa lilipatikana kupitia kwa beki,Branislav Ivanovic aliyeonyesha juhudi binafsi katika dakika ya 45.
Huku ikionekana kama uongozi huo wa goli moja unatosha kuwasogeza kileleni kwa pointi nne zaidi katika msimamo wa ligi kuu ya Uingereza lakini Victor Anichebe aliyetokea benchi alifunga goli la kusawazisha zikiwa zimebaki dakika tatu mpira kumalizika.

Mourinho amekataa kusema kuwa sare hiyo imepoteza nafasi muhimu kwa timu yake katika kuongeza gepu la pointi lakini akakiri kuwa muda pekee ndiyo utasema kuwa wamepoteza pointi muhimu au wamepata pointi muhimu.
Akisisitiza kuwa,”Pointi ni pointi na hivyo tusubiri kuona mwisho wa msimu kama tumepoteza pointi mbili au tumeshinda moja.”
Mreno huyo aliwasifia wapinzani wake na kusema kuwa katika 20 za mwisho waliwaweka katika presha kubwa na kufanikiwa kusawazisha goli hivyo labda walistahili kupata pointi.

Ila akasema kwenye dakika 60 za mwanzo walimiliki sana mpira ingawa sio kwa kiasi kikubwa ila waliwazidi wenyeji karibu kila idara.
Manchester City na Arsenal watatumia nafasi hiyo kutaka kupunguza uwiano wa pointi na labda kupanda kileleni watakapo shuka dimbani leo( Jumatano) lakini Mourinho alikataa kutazama sana hali hiyo akidai kuwa anaangalia mechi baada ya mechi.
Pia akaongeza kuwa wana mchezo ujao dhidi ya Everton na wanapaswa kujaribu kushinda na kupata pointi zote tatu hakuna kingine zaidi ya hicho.

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog