Wednesday, February 12, 2014


Jumla ya wachezaji na viongozi 30 wa klabu ya Yanga watasafiri kwenda visiwa vya Komoro kucheza mchezo wa marudiano katika michuano ya klabu bingwa Afrika. Kikosi kamili cha wachezaji wa Yanga watakao ondoka ni kama ifuatavyo;  Magoikipa ni: Deogratias Munish "Dida" na Ally Mustafa "Barthez". Walinzi: Juma Abdul, Mbuyu Twite, Oscar Joshua, David Luhende, Nadir Haroub "Cannavaro", Kelvin Yondani na Rajab Zahir. Viungo: Athuman Idd "Chuji", Frank Domayo "Chumvi", Haruna Niyonzima, Hassan Dilunga na Hamis Thabit. Washambuliaji: Hamis Kiiza, Didier Kavumbagu, Said Bahanuzi, Saimon Msuva na Mrisho Ngasa 

Kikosi hiki cha Yanga kinatarajia kupaa kesho (trh 13 Feb) saa sita mchana na kinatarajia kucheza mechi yake ya marudiano siku ya jumamosi dhidi ya Komorozine de Domoni kwenye uwanja wa Stade International Said Mohamed Cheik Mitsamiouli. 

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog