Wednesday, February 12, 2014



Meneja wa Chelsea,Jose Mourinho anatabiri kuwepo kwa mianya mibovu katika mchezo wa soka mara baada ya Yaya Toure kukwepa adhabu ya wazi Jumatatu.
Kiungo huyo wa Manchester city alionekana akimkanyaga kwa makusudi mshambuliaji wa Norwich City,Ricky van Wolfswinkel katika mchezo wa ligi kuu ya Uingereza Jumamosi katika uwanja wa Carrow Road katika tukio ambalo mwamuzi,Jon Moss hakuliona uwanjani.
Ilikuwa ni maamuzi yanayotakiwa kuamuliwa mara baada ya kutumia tekinolojia mpya ya picha za video iliyowekwa na Chama cha soka,FA kuamua tukio hilo na kufanya maamuzi lakini hakukuwa na uwamuzi wowote uliofanywa .
Mourinho baada ya adhabu kutupiliwa mbali alionya kuwa kukosa adhabu kwa Toure,kutapeleka ujumbe kwa wachezaji wengine kuwa huru kufanya kitu chochote uwanjani ambacho hakiwezi kuonekana moja kwa moja kwani hawatachukuliwa hatua zozote.
Mreno huyo alisisitiza kuwa,”Kama Toure hajachukuliwa hatua ni wazi kuwa wachezaji sasa wanaweza kufanya tukio lolote baya uwanjani ambalo mwamuzi hawezi kuona.”
Na kuongeza kuwa,”Kama wametengeneza tekinolojia ya kamera wanapaswa kutumia sheria hiyo iwapo mwamuzi hataona baadhi ya matukio.”
Mourinho alizungumza hayo kabla ya FA hawajachukua hatua zozote kwa Toure na mara baada ya maamuzi kufanywa raia huyo wa Ivory Coast atakuwa huru kucheza mchezo wa Kombe la FA dhidi ya Chelsea Jumamosi ikiwa ni raundi ya tano.

Mchezaji aliyefanyiwa madhambi raia wa Uholanzi,Van Wolfswinkel alionyesha kuridhika kutokana na Toure kusalimika na adhabu akiandika katika mtandao wa kijamii kuwa,”Ni vizuri kumuona Toure hajapewa adhabu,wachezaji kama yeye ni mali ya uwanja!Kilichotokea Carrow Road kinabaki Carrow Road.”

Akaongeza kuwa,”Matukio mengi kama hayo yanatokea uwanjani lakini watu wote tunafurahia kumuona Toure  akicheza soka hivyo inapaswa uchukulie kama ilivyo na ufurahie soka na ndivyo ilivyo.

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog