Wednesday, February 12, 2014

Fowadi wa Arsenal Yaya Sanogo atakuwa dimbani leo wakati ambapo washika bunduki hao wa London watakapowakaribisha Manchester United baada ya fowadi huyo kuwa nje kwa kipindi cha miezi mitano ya kuuguza mgongo.
Mathieu Flamini amekamilisha mechi tano alizofungiwa, wakati Aaron Ramsey, Kim Kallstrom, Thomas Vermaelen, Abou Diaby na Theo Walcott wakiwa bado wagonjwa.
Mapacha wawili wa Manchester United Phil Jones na Jonny Evans watakosa mchezo wa leo

 kutokana na kuumia huku kiungo Marouane Fellaini akiendelea kuwa nje.
Mechi nyingine za leo ni Everton watakuwa wenyeji wa Crystal Palace, Man City watakuwa wenyeji wa Sunderland na Newcastle wataikaribisha Tottenham.
Stoke City na Swansea wakati Fulham watakuwa kibaruani nyumbani dhidi ya Liverpool.

Jumatano Februari 12
22:45 Arsenal v Man United
22:45 Everton v Crystal Palace
22:45 Man City v Sunderland
22:45 Newcastle v Tottenham
22:45 Stoke v Swansea
23:00 Fulham v Liverpool

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog