Thursday, July 31, 2014


Mkurugenzi wa bendi, Isha Mashauzi akilikabili jukwaa vilivyo.
Bendi ya Taarab inayokimbiza mjini, Mashauzi Classic usiku wa kuamkia leo ilikamua kinoma katika ukumbi wa Lina's Night Club Bukoba Mjini. Kiongozi wa Mashauzi Classic, Isha Makongo akiliongoza kundi lake kutoa burudani katika Ukumbi wa Lina's Night Usiku huuBaadhi ya Waimbaji wa Kundi hilo la Mashauzi Classic wakiwajibika jukwaani kutoa burudani kwa Mashabiki wao.Kikosi kizima cha Mashauzi Classic kikifanya mashambulizi jukwaani.

Isha Makongo akiimba mbele ya Waimbaji wake Jukwaani kuwapa raha mashabiki wao wa bukoba usiku huu.
Hashim Said mwimbaji kiongozi msaidizi akifanya yake

Kundi la Mashauzi Classic Modern Taarab, usiku wa kuamkia leo liliwanogesha mashabiki wake katika onesho lililofanyika Ukumbi wa Lina's Night Club Bukoba na Kushuhudiwa na Watu wengi waliojitokeza kwa Wingi katika Ukumbi huu.
Mashabiki wa bendi hiyo wakiburudika kwa nyimbo za Taarab kutoka kwa Bendi hiyo ya Mashauzi Classic kwa  raha zao.


Capello to stay on as Russia boss until 2018


LICHA ya kuboronga kombe la dunia majira ya kiangazi mwaka huu nchini Brazil, Fabio Capello ataendelea kuwa kocha wa timu ya taifa ya Urusi mpaka 2018 .
Waziri wa michezo wa nchi hiyo, Vitaly Mutko amemtania kuwa kama atatwaa kombe la dunia lijalo, atazikwa sehemu aliyozikwa mwandishi gwiji, Fyodor Dostoyevsky.
Muitaliano huyo aliiongoza nchi hiyo ya Ulaya mashariki katika mashindano ya kombe la dunia, lakini alitupwa nje hatua ya makundi ambapo alikuwa na timu za Ubelgiji, Korea Kusini na Algeria.
Hata hivyo, Capello ataendelea kuwa kocha mkuu mpaka 2018 wakati ambao Urusi itakuwa mwenyeji wa fainali zijazo za kombe la dunia na Vitaly Mutko anasema anayo nafasi ya kushinda mioyo ya watu wa Urusi.
“Kama tutafanikiwa kwenye mashindano ya mwaka 2018, tutamzika karibu na Dostoyevsky,” aliwaambia waandishi wa habari.
Wakati huo huo, Capello anajiandaa na michuano ya mataifa ya Ulaya mwaka 2016, lakini amekiri kuwa kipaumbele chake ni fainali za kombe la dunia 2018.

“Lengo kubwa ni kombe la dunia, lakini kwanza tunatakiwa kufuzu michuano ya Ulaya mwaka 2016 nchini Ufaransa,” alisema.

433211_heroa 
NEYMAR ameweka wazi kuwa atarudi uwanjani agosti 18 mwaka huu kuitumikia Barcelona katika mechi ya maandalizi ya kabla ya msimu ya kombe la Joan Gamper dhidi ya Leon.
Mbrazil huyo alivunjika mfupa wa uti wa mgongo wakati wa mechi ya robo fainali ya kombe la dunia dhidi ya Colombia na alizikosa mechi mbili.
Neymar aliwakosa Ujerumani, hatua ya nusu fainali na Uholanzi mechi ya mshindi wa tatu.


Mwanamuziki nyota wa Bongo Fleva, Khalid Mohammed ‘TID Mnyama’ akizikonga nyoyo za mashabiki wa Dar Live katika Usiku wa Mnyama na Wanyama.
Mnyama TID akijiachia kwa mashabiki wake wa Dar Live.
Mwanamuziki Jafarai akipagawisha mashabiki waliofurika katika Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live.
Jay Moe akifanya makamuzi katika steji ya kupanda na kushuka ya Dar Live.
Inspector Haroun akiwapa hi mashabiki wake ndani ya Dar Live.
Mwanadada Naaziz kutoka Kenya akilishambulia jukwaa la Dar Live.
Masai Sharo akifanya vitu vyake stejini.
Mashabiki wakijiachia kijanja ndani ya Dar Live.
TID akitunzwa Cheni na shabiki wake.
TID akifanya manjonjo yake mbele ya Naaziz.
Nyomi ikifuatilia burudani za Idd Pili ndani ya Dar Live.


WACHEZAJI WA COASTAL UNION U-20 WAKIWA UWANJANI NA AFRICAN SPORTS


MAKAMU MWENYEKITI WA COASTAL UNION STEVEN MGUTO KULIA AKIWA NA MJUMBE WA KAMATI YA UTENDAJI YA COASTAL UNION SALIMU AMIRI KUSHOTO

MAKAMU MWENYEKITI WA COASTAL UNION STEVEN MGUTO AKIWA NA MWAVULI AKIANGALIA MECHI YA COASTAL UNION U 20 NA AFRICAN SPORTS HUKU MVUA IKIENDELEA KUNYESHA KWENYE UWANJA WA MKWAKWANI LEO

MAKAMU MWENYEKITI COASTAL UNION STEVEN MGUTO KUSHOTO AKIBADILISHANA MAWAZO NA MWENYEKITI WA CHAMA CHA SOKA MKOA WA TANGA SAID SOUD LEO WA KWANZA KULIA NI KATIBU WA CHAMA CHA SOKA MKOA WA TANGA,BEATRICE MGAYA

WAJUMBE WA KAMATI TENDAJI COASTAL UNION SALIM AMIRI KUSHOTO NA SALIM BAWAZIRI KULIA WAKIFUATILIA MCHEZO HUO



KOCHA MKUU WA COASTAL UNION YUSUPH CHIPO KULIA AKITOA MAWAIDHA KWA WACHEZAJI WA KIKOSI CHA U 20 LEO


WA KWANZA KULIA NI KOCHA MSAIDIZI WA COASTAL UNION BENARD MWALALA ANAYEFUATIA NI KOCHA MKUU YUSUPH CHIPPO WAKIANGALIA MAWAIDHA YANAYOTOLEWA NA KOCHA WA U 20 JOSEPH LAZARO LEO



 Na Boniface Wambura, Johannesburg


Kikosi cha Taifa Stars kimewasili salama jana (Julai 30 mwaka huu) hapa Johannesburg kwa ajili ya maandalizi ya mwisho kabla ya kwenda Maputo, Msumbiji kwa ajili ya mechi dhidi ya Mambas itakayochezwa Jumapili.
Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager imefanya mazoezi mara mbili leo- asubuhi na jioni kwenye uwanja wa Bedfordview Country Club. Mazoezi ya mwisho yatafanyika kesho asubuhi (Agosti 1 mwaka huu) kabla ya baadaye jioni kuanza safari ya Maputo.
Wakati huo huo, Balozi wa Tanzania hapa Afrika Kusini, Razia Msuya baadaye leo jioni atazitembelea timu zote mbili za Tanzania zilizopo hapa Johannesburg kusalimia wachezaji.

Serengeti Boys yenyewe ipo hapa tangu Julai 27 kwa ajili ya mechi dhidi ya Afrika Kusini itakayochezwa Jumamosi (Agosti 2 mwaka huu).


Chelsea imeichapa Vitesse Arnhem ya Uholanzi kwa mabao 3-1 katika mechi ya kirafiki iliyochezwa.
Lakini mechi hiyo ilikuwa na rekodi kadhaa, mfano Cesc Fabregas akianza kuifungia Chelsea bao la kwanza katika hayo matatu, mabao mengine yalifungwa na Mo Salah, Nemanja Matic.

Diego Costa ambaye alitengeneza mabao yote matatu alitaka kuzichapa uwanjani na beki wa Vitesse, Guram Kashia akimtuhumu kumchezea rafu mbaya kwa makusudi.
Mshambuliaji aliyerejea Chelsea, Didier Drogba aliendelea kubaki kwenye benchi akishuhudia Chelsea ikiendelea na mechi za kirafiki.






waliotembelea blog