Saturday, February 8, 2014

article-2553471-03C02EE60000044D-546 634x4311 e9280
BEKI wa Manchester United, Nemanja Vidic ametangaza kuondoka katika klabu hiyo mwishoni mwa msimu huu baada ya kukataa kuongeza Mkataba.
Kocha David Moyes alikuwa tayari kumbakiza Nahodha wake huyo Old Trafford, lakini Vidic, anayemaliza Mkataba mwishoni mwa msimu, ameamua kuondoka baada ya kuitumikia Manchester kwa miaka minane.
Mserbia huyo ameshinda mataji 15 tangu awasili klabu hiyo akitokea Spartak Moscow ya Urusi kwa ada ya uhamisho ya Pauni Milioni 7, Januari mwaka 2006, na baadayekuwa Nahodha chini ya kocha Sir Alex Ferguson.
Katika taarifa yake, Vidic amesema: "Ni mwaka wa mwisho wa Mkataba wangu na nimekuwa na miaka minane mizuri hapa. Chanzo: binzubeiry

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog