Saturday, February 8, 2014

779E6803-5815-43C8-94E9-1E5BCA636EF4 w640 r1 s1 1bc94
Rais Barack Obama anasema uhuru wa kuabudu ni muhimu katika ulinzi wa kitaifa na kwamba Marekani inaunga mkono uhuru sawa na huo nje ya nchi kama mojawapo ya sera zake muhimu za kigeni.
Bw. Obama alikuwa akizungumza Alhamis wakati wa dhifa ya kila mwaka ya maombi ya kitaifa jijini Washington, ambako alisema yeyote anayemdhuru mwingine kwa kutumia imani ya dini anadhulumu uhusiano wake mwenyewe na Mwenyezi Mungu.
Aliwasihi walioshiriki katika mamombi hayo kuwaombea wote waliokamatwa na kuzuiliwa kutokana na imani zao za kidini, akiwemo Kenneth Bae aliyezuiliwa Korea Kaskazini na Saeed Abedini aliyezuiliwa huko Iran.
Maombi ya kitaifa ya kila mwaka huandaliwa na wabunge wa Marekani katika majengo ya bunge. Na kila rais wa Marekani amehudhuria maombi hayo tangu yalipoanza mwaka wa 1953. Chanzo: voaswahili

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog