Saturday, February 8, 2014

10 386c2
KOCHA Manuel Pellegrini ameshina tuzo ya kocha bora wa mwezi Ligi Kuu ya England, baada ya Manchester City kuweka rekodi nzuri Januari ikishinda mechi nne kati ya nne.
Huu ni mwezi wa pili mfululizo Pellegrini anashinda tuzo hiyo - na mara ya kwanza kwa kocha mmoja kushinda mara mbili mfululizo tangu Carlo Ancelotti afanye hivyo akiwa kocha wa Chelsea mwaka 2011.
Nyota wa Sunderland, Adam Johnson ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa mwezi wa Ligi Kuu baada ya kazi nzuri aliyoifanya mwezi uliopita akifunga mabao matano. Chanzo: binzubeiry

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog