Saturday, February 8, 2014

Arsenal-v-Liverpool1 62df8
London, England. Vinara wa Ligi Kuu England, Arsenal leo wanaanza kuruka viuzi vizito vya Februari wakati wakapokuwa ugeniniAnfield kucheza mechi yake ya kwanza kati ya mbili dhidi ya Liverpool katika wiki hii.
Nafasi ya kikosi cha Arsene Wenger kumaliza ukame wa miaka minane bila ya taji itajulikana vizuri mwisho wa mwezi huu.
Wana mechi ya nyumbani ya Ligi Kuu dhidi ya Manchester United, na Kombe la FA dhidi ya Liverpool pamoja na mechi mbili za hatua ya 16 bora za Ligi ya Mabingwa dhidi ya Bayern Munich zitafutia baada ya mechi ya leo, na endapo watapoteza basi watakosa nafasi ya kutwaa moja ya mataji hayo matatu.
Arsenal wanaongoza ligi kwa tofauti ya pointi mbili kwa Manchester City, ambao wenyewe watacheza na Norwich City na Chelsea walio nafasi ya tatu watakuwa nyumbani kucheza dhidi ya Newcastle United na kipigo cha Gunners ndani ya Anfield kitawashusha hadi nafasi ya tatu.
Kama Liverpool watafungwa leo wataachwa nyuma kwa pointi 11 na vinara hao.
Wapinzani wa Liverpool katika kuwania nafasi ya nne, Tottenham Spurs, Everton na Manchester United watashuka uwanjani kesho.
Manchester United watakuwa na kibarua kizito mbele Fulham. Huku Spurs watawakaribisha Everton katika mechi za kusaka kucheza Ligi ya Mabingwa msimu ujao. Chanzo: mwananchi

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog