Saturday, February 8, 2014

 

KLABU ya Manchester City imepanga kuongeza Uwanja wake wa Etihad kwa zaidi ya viti 14,000 ambapo mara baada ya mpango huo kukamilika uwanja huo utakuwa na uwezo wa kuingiza mashabiki 62,170 badala ya 47,620 kama ilivyo sasa. Mpango huo tayari umeshawasilishwa katika tume ya mipango ya halmashauri na kutokana na ripoti iliyotolewa jana mpango huo umekubaliwa. Kama matengenezo ya uwanja huo yakiendelea jiji la Manchester litakuwa na viwanja viwili vikubwa nchini Uingereza mwingine ukiwa ni Old Traford. Man City wamefikia mpango huo ili kuongeza mapato katika viingilio hususani katika kipindi hiki ambacho timu hiyo inafanya vyema katika michuano mbalimbali ya ndani na kimataifa.Etihad Stadium itakavyoonekanaMwonekano safi wa EtihadMchoro mpya wa uwanja wa  Etihad
North to South

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog