Saturday, February 8, 2014

ronaldo fcace
REFA aliyemuonyesha kadi nyekundu Cristiano Ronaldo wakati Real Madrid ikitoa sare na Athletic Bilbao mwishoni mwa wiki iliyopita amefungiwa kwa sababu za kuvurunda katika maamuzi yake.
Kamati ya Ufundi ya Marefa Hispania (CTA) limemfungia kwa mwezi mmoja Miguel Angel Ayza Gamez na hataruhusiwa kabisa kuchezesha mechi za Real msimu huu.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka Hispania, kuna hatari zaidi akaondolewa kabisa katika orodha ya marefa wa La Liga kutokana na madudu aliyoyafanya katika mechi hiyo.
Ronaldo alitolewa nje kwa mara ya saba katika historia yake ya soka dakika ya 75 siku hiyo timu hizo zikifungana 1-1 Uwanja wa San Mames baada ya kumuinulia mkono Nahodha wa Bilbao, Carlos Gurpegi, ambaye alijiangusha.
Pia alimvaa kiungo wa Bilbao, Ander Iturraspe wakati akiwa na hasira za tukio hilo.
Inafahamika taarifa ya awali ya Ayza Gamez ilisema alimtoa nje Ronaldo kwa tulio alilolifanya kwa Gurpegi, lakini baadaye akabadilisha na kusema alimtoa nje kwa kosa la kumsukuma Iturraspe - maneno ambayo yalisemwa na mchezaji huyowa Bilbao. Chanzo: binzubeiry

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog