Saturday, February 8, 2014


3 
Na watenda kazi Francis Godwin Blog ,Njombe na Iringa
WAKATI  wananchi  wa kata ya  Nduli jimbo la Iringa mjini na  wale  wa kata ya Njombe mjini  jimbo la Njombe  kusini  kesho wanashiriki katika zoezi la upigaji  kura katika  uchaguzi mdogo  wa udiwani ,chama  cha mapinduzi (CCM ) mkoa  wa  Iringa na Njombe  kimelaani  vurugu  zinavyofanywa na viongozi na  wafuasi  wa Chadema katika chaguzi hizo na  kuwaomba  wananchi kujitokeza  kwa wingi katika uchaguzi  huo bila vitisho na kuchagua wagombea  wa CCM.
Huku  jeshi la  polisi Imkoa  wa Njombe likidai limejipanga kwa ulinzi polisi mkoa  wa Iringa limedai   kuwa  kuna  kikundi  kinasakwa kwa  kutaka  kufanya  vurugu katika uchaguzi huo na kuwaondoa  hofu  wananchi kufika  kupiga kura  bila kuogopa .
Kaimu  katibu  wa CCM mkoa  wa Iringa Hassan Mtenga  alitoa kauli hiyo jana  wakati wa ufungaji wa kampeni  za uchaguzi mdogo kata ya  Nduli  jimbo la Iringa  mjini .
Alisema  kuwa  lengo la chama  chochote cha siasa ni  kuona  wananchi  wake  wanaendelea  na shughuli  zao katika hali ya amani na utulivu   na  kuwa chama  chochote cha siasa  kinachojihusisha na vitendo vya  kinyama dhidi ya wananchi  wake ni wazi hakipo kwa  ajili ya kulinda amani ya wananchi.
Hivyo  alisema vurugu zilizofanywa na wafuasi wa Chadema na mbunge  wa  jimbo  hilo la Iringa mjini mchungaji Peter Msigwa  juzi ni  wazi kuwa Chadema hakipendi kuna wananchi  wakifanya shughuli  zao kwa amani  na kutokana na unyama  huo  unaofanywa na Chadema ni vema  wana Nduli kuendelea kuchagua  CCM ili amani  iliyopo izidi kulindwa . Mtenga  alisema mbali ya CCM kuruhusu  vyama  vingi vya  siasa  mwaka 1994 ila bado baadhi ya  vyama  vya siasa  vimekuwa ni mwanzo  wa  kuvuruga amani ya watanzania na  kuwa ni vyama vya  kusababisha  vurugu  hata mauwaji kwa  watanzania .
Alisema  kuwa haiwezekani  kwa  chama makini chenye kupenda  amani  kuona kinashabikia vurugu  na hata  wabunge  wake  na  viongozi  wake kila kukicha  wakikamatwa kwa  vurugu katika mikutano.
Mtenga  alisema  jimbo la Iringa mjini limeendelea kuzolota katika maendeleo  kutokana na vurugu  za kisiasa za mara kwa mara  zinazojitokeza na  kuwa hata  maendeleo  yanayoonekana kama huduma ya maji  safi kwa wananchi wa Nduli ni  jitihada za mbunge wa  wa CCM aliyekuwepo kabla ya Msigwa pamoja na mbunge viti maalum mkoa  wa Iringa Ritta Kabati ambae  kila  wakati bungeni amekuwa akipigania .
“Tunapenda  kuwahakikishia  wana Nduli  kuwa  iwapo  mtatuwekea mrithi  wa diwani  marehemu Iddi Chonanga  kutoka  CCM pale  alipoishia  diwani  wenu katika maendeleo pataendelezwa  zaidi  kwani  mwenye  kukabidhiwa  mikoba ya diwani  aliyekufa ni lazima awe  kutoka  CCM na si vinginevyo”
Kwa  upande  wake  Chama  cha  Mapinduzi mkoa  wa Njombe kimeeleza  kusikitishwa na vurugu  mbali mbali  zinazojitokeza katika kampeni  za udiwani kata ya  Njombe mjini baada ya  wafuasi na viongozi wa Chadema  kuwapiga wananchi .
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Njombe Deo Sanga ambae ni mbunge wa  jimbo la Njombe Kaskazin  alisema kuwa siasa  inayofanywa na  wana Chadema kwa Njombe mjini ni siasa ya kinyama na kuwa ilipendeza kwa vyama vya  siasa  kushindana kwa sera na hoja badala ya  kushindana kwa vurugu .
HIvyo  alisema  kuwa ili  CCM kuendelea  kutimiza ahadi zake na kuongoza kata  hiyo ni  wajibu wa  wananchi wa Njombe kuchagua mgombea wa CCM badala ya  kuwasikiliza wafuasi hao wa Chadema kutoka nje ya Njombe ambao wapo kwa ajili ya kutaka kuvuruga uchaguzi  huo.
Huku mbunge  wa  jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe akiwataka  wana Njombe mjini  kutokubali  kata   hiyo ya Njombe mjini  kuchukuliwa na vyama vya upinzani na  kuwataka  kuchagua chama  cha mapinduzi.
Filikunjombe  alitoa kauli hiyo  wakati wa kumnadi mgombea  udiwani wa CCM katika kata  hiyo ya Njombe mjini na  kuwa Wilaya ya  Ludewa na Njombe ni wilaya  majirani na  kuwa  masilimali za  Ludewa ambazo ni makaa ya mawe na Liganga si tu ukombozi kwa  wana Ludewa ni ukombozi wa mkoa wa Njombe na Taifa  hivyo kuwataka  vijana  kuendelea  kuwa na imani na serikali ya chama cha mapinduzi chini ya Rais Dr Jakaya  Kikwete ambae katika utawala  wake watanzania  wanashuhudia miradi hiyo mkikubwa  inaanza.
Alisema  kuwa uchumi  wa Njombe na Ludewa  baada ya kuanza kwa miradi  hiyo utakuwa  zaidi kutokana na vijana  wengi kupata ajira katika  miradi hiyo. Wakati  huo  huo Jeshi la  polisi  mkoa  wa Njombe na Iringa  limesema  limejipanga  vyema  kwa ulinzi wakati wa  zoezi nzima la upigaji  kura  hadi kutangazwa kwa matokeo  ya uchaguzi na kuwa  atakayejaribu  kumtisha mpiga kura  asifike  kupiga  kura atakiona cha moto kutoka kwa  jeshi  hilo.
Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Njombe Fulgence Ngonyani akizungumza na mwandishi wa habari hizi kwa  njia ya simu jana alisema  kuwa  jeshi  lake  limefanikiwa  kuwapa mafunzo maalum askari  wake kwa ajili ya kulinda amani wakati wa zoezi la uchaguzi huo na  kuwataka  wananchi wa Njombe mjini wenye sifa ya  kupiga kura  kufika kupiga  kura bila kitisho  kutoka kwa  mtu yeyote na kuwa yule atakayetishwa asisite  kutoa taarifa kwa askari  watakaokuwepo maeneo yanayozunguka vituo  vya kupigia kura.
Huku kamanda wa  polisi  mkoa wa Iringa Ramadhan Mungi akisema  kuwa  jeshi lake  limejipanga  toka mwanzo katika kampeni hizo.
Kamanda  Mungi  alisema  kuwa kumekuwepo na  vurugu  za hapa na pale ambazo zinatokana na pambe  moja kati ya  zinazovutana  kukata  tamaa katika uchaguzi huo  kutokana na kujijipanga  vema japo  wao kama polisi wamejipanga  kuona  amani na utulivu  unakuwepo wakati  wote wa upigaji kura na utangazaji wa matokeo japo alisema  zipo  taarifa  za  baadhi ya  wafuasi wa moja kati ya  vyama  vya  siasa  kupanga  kufanya vurugu  na kuwa tayari  kikundi  hicho  kinajulikana na  wameanza msako  wa kukisaka  ili  kufikishwa katika vyombo  vya sheria.
Joto  hilo la uchaguzi  mdogo katika kata ya Nduli linaonyesha kwenda  vibaya   zaidi kwa Chadema  kutokana na mgombea aliyesimamishwa Ayub Mwenda awali alipata  kuwa mwenyekiti wa serikali ya  kijiji  cha Nduli na kutolewa na  wananchi kwa kura  za maoni za kutokuwa na imani nae  kutokana na madai ya  kula fedha za kijiji na baada ya  hapo  kuamua  kuhamia Chadema na kuchukua fomu ya  kuwania nafasi hiyo ya udiwani jambo ambalo  wanadai  kuwa kupata udiwani katika kata  hiyo ni vingumu  zaidi .
Pia  uchaguzi huo  ni kipimo  moja wapo  kwa mbunge wa jimbo la Iringa mjini mchungaji Peter Msigwa kama bado anakubalika ama  lah ila  pia  ni kipimo  kwa CCM kuendelea  kushinda chaguzi za serikali za mitaa na uchaguzi mkuu 2015 .
Hali katika kata ya Njombe mjini upepo wa kisiasa hadi  sasa ni 50 kwa 50 kwa vyama viwili  vilivyojitokeza CCM na Chadema ambapo  kuna  uwezekano  wa CCM kushinda tena kwa  kumrudisha  diwani wa CCM ama  kushindwa kutokana na vyama hivyo  viwili  kuonyesha  kukamiana  kupita kiasi.

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog