Kesho jumapili, Rio Ferdinand atarudi katika klabu yake ya zamani, Manchester United akiichezea Queens Park Rangers
RIO Ferdinand anarudi Manchester United
kwa mara ya kwanza kesho jumapili, lakini amelalamika kuwa klabu hiyo
aliyoichezea kwa miaka 12 kamwe haikumpa nafasi ya kuaga kabla ya
kujiunga na QPR.
Ferdinand aliichezea United mechi 455 na
alitoa mchango mkubwa katika mafanikio ya Sir Alex Ferguson, lakini
Mkurugenzi msaidizi Ed Woodward alimuambia baada ya mechi ya mwisho
dhidi ya Southamptom msimu uliopita kuwa hataongezewa mkataba.
Baada ya kuambiwa hivyo, beki huyo mwenye miaka 35 aliondoka Old Trafford na kujiunga na QPR mwezi julai mwaka huu.
"Nilikuwa na mafanikio makubwa Old
Trafford," alisema Ferdinand. "Sijawahi kupata nafasi ya kuaga
nilipoondoka. kilikuwa kitendo kibaya, kwahiyo nitapata fursa ya kuwaaga
watu wengi walionisapoti na kunisaida"
Beki huyu alijiunga na Harry Redknapp katika dimba la Loftus Road majira ya kiangazi baada ya kutumika kwa miaka 12 Old Trafford
Ferdinand aliiwakilisha vyema Manchester United kwa muongo mmoja na alibeba makombe sita ya ligi kuu
0 maoni:
Post a Comment